• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  MOURINHO AMVULIA KOFIA DROGBA AKIPOEKEA TUZO

  KOCHA Jose Mourinho amemwagia pongezimshambuliaji mkongwe, Didier Drogba jioni ya Jumapili kwa tuzo yake ya heshima alitopewa na Chama cha Waandishi wa Habari za soka.
  Deogba amepewa tuzo ya mchango wa muda mrefu katika mchezo na kocha wa The Blues amesema nyota huyo wa Ivory Coast aliyetua kwa mara ya kwanza Chelsea kwa dau la pauni Milioni 24 mwaka 2004, ndiye mchezaji bora daima katika historia ya klabu.
  Kocha huyo Mreno alisema hayo katika usiku wa tuzo za FWA ukumbi wa Savoy, HOTEL LONDON.
  Akiwa amevalia nadhifu, suti ya bluu na tai, mshambuliaji huyo mkongwe alifuata nyayo za Mourinho, Sir Alex Ferguson na David Beckham katika kushinda tuzo hiyo.
  Chelsea striker Didier Drogba poses with his award at the Football Writers' Association Gala Tribute evening
  Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba akiwa amepozi na tuzo yake Waandishi wa Habari za soka katika hafla hiyo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2925836/Didier-Drogba-honoured-Football-Writers-Association-Jose-Mourinho-hails-striker.html#ixzz3PsH1w0f8 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO AMVULIA KOFIA DROGBA AKIPOEKEA TUZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top