• HABARI MPYA

  Tuesday, January 27, 2015

  BORO WALIOING'OA MAN CITY KOMBE LA FA WAPEWA ARSENAL RAUNDI YA TATU, MAN UNITED...

  TIMU ya Middlesbrough wamepata zawadi ya ushindi wao wa Kombe la FA Jumamosi dhidi ya mabingwa wa England, Manchester City Uwanja wa Etihad baada yaa kupanhiwa vigogo wengine, Arsenal katika Raundi ya Tatu.
  Timu hiyo ya Daraja la Kwanza, ilishinda 2-0 dhidi ya kikosi cha Manuel Pellegrini katika Raundi ya Nne - shukrani kwao wafungaji Patrick Bamford na Kike - na sasa wataifuata The Gunners Uwanja wa Emirates katika hatua ijayo ya mashindano hayo.
  Wakati huo huo, mshindi wa mchezo wa marudio wa Raundi ya Nne kati ya Manchester United  na Cambridge ya Daraja la Pili, ambazo zilitoka sare Ijumaa atasafiri kuifuata Preston au Sheffield United.
  Arsenal will host Middlesbrough in the fifth round of the FA Cup after beating Brighton on Sunday
  Arsenal itamenyana na Middlesbrough katika Raundi ya Tatu KOmbe la FA 

  RATIBA KAMILI KOMBE LA FA RAUNDI YA TATU...

  Crystal Palace vs Liverpool or Bolton Wanderers
  Arsenal vs Middlesbrough
  Aston Villa vs Leicester City
  West Brom vs West Ham
  Bradford City vs Sunderland or Fulham
  Blackburn Rovers vs Stoke City
  Derby County vs Reading
  Preston North End au Sheffield United vs Cambridge United au Manchester United
  Mechi zitachezwa wikiendi ya Februari 14 na 15 mwaka 2015.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORO WALIOING'OA MAN CITY KOMBE LA FA WAPEWA ARSENAL RAUNDI YA TATU, MAN UNITED... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top