• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  KUNDI D BALAA AFCON, CAMEROON NAYO SARE SARE 1-1 NA GUINEA


  Cameroon imelazimishwa sare ya 1-1 na Guinea katika mchezo wa Kundi D Kombe la Mataifa ya Afrika, Uwanja wa Malabo, Equatorial Guinea. Benjamin Moukandjo alianza kuwafungia Simba Wasiofungika dakika ya 13, kanla ua Ibrahima Traore kuisawazishia Guinea dakika ya 42. Matokeo hayo yanazidi kulifanya kundi hilo liwe gumu kutoa timu za kwenda hatua ya pili, baada ya timu zote kutoa sare katika mechi zote, hivyo kila moja ina poingi mbili mabao mawili baada ya mechi mbili.
  Sasa mechi za mwisho za kundi hilo ndizo zitaamua timu mbili za kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, Cameroon ikimaliza na Ivory Coast na Guinea na Mali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KUNDI D BALAA AFCON, CAMEROON NAYO SARE SARE 1-1 NA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top