• HABARI MPYA

  Friday, January 23, 2015

  SITA ZAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  TIMU za mikoa sita tayari imepata tiketi za kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake itakayoanza Januari 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati nyingine mbili zinajulikana leo (Januari 23 mwaka huu).
  Mikoa ambayo timu zake tayari zina tiketi za robo fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin ni Ilala, Kigoma, Mwanza, Pwani, Tanga na Temeke.
  Kiungo wa Mwanza, Nabila Ahmad Hazaa, timu yake imefuzu Robo Fainali

  Matokeo ya mechi za leo kati ya Iringa na Ruvuma, na ile kati ya Mbeya na Katavi ndiyo yatakayoamua ni timu zipi mbili kati ya hizo zinakwenda Dar es Salaam kucheza robo fainali.
  Timu zote zilizofuzu hatua ya robo fainali zinatakiwa kuripoti Dar es Salaam keshokutwa (Januari 25 mwaka huu). Fainali ya michuano hiyo itachezwa Februari Mosi mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SITA ZAFUZU ROBO FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top