• HABARI MPYA

  Saturday, January 24, 2015

  BAO WALILOLALAMIKIA YANGA KUNYIMWA NA KANYENYE LEO MOROGORO

  Kipa Tony Kavishe akiwa amedaka mpira mbele ya wachezaji wa Yanga SC, nyuma ya mabeki wake. Ni moja kati ya nafasi nzuri za kufunga mabao zaidi walizopoteza Yanga SC katika ushindi wao wa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Wachezaji wa Yanga walilalamika kwamba kipa huyo alidakia ndani kiasi cha kumfuata refa.
  Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' kulia akizungumza na mshika kibendera namba moja, John Kanyenye wa Mbeya kulalamika kunyimwa bao. Kushoto ni kiungo Mbrazil wa timu hiyo, Andrey Coutinho. Awali, refa Ahmada Simba wa Kagera alinyoosha mkono wake kati akiashiria ni bao, lakini Kanyenye akamuita kumuambia si bao. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAO WALILOLALAMIKIA YANGA KUNYIMWA NA KANYENYE LEO MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top