• HABARI MPYA

  Thursday, January 29, 2015

  TEMEKE YAWASHUGHULIKIA KISAWASAWA ‘MASISTADUU’ WA ILALA KOMBE LA TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TEMEKE imeinyanyasa Ilala katika Nusu Fainali ya Kombe la Taifa kwa Wanawake baada ya kuitandika mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Temeke wakiwa katika viunga vya nyumbani, wakishangiliwa na mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani, waliifunika kabisa Ilala jioni ya leo na sas
  Mfungaji wa mabao mawili ya Temeke leo, Neema Paul akishangilia moja ya mabao yake na chini wachezaji wa Temeke wakishangilia ushindi wao wa kishindo 
  a watakutana na Pwani katika Fainali Jumapili.
  Neema Paul alifunga mabao mawili ya Temeke katika mchezo huo, dakika ya 12 na 62, wakati mabao mengine yalifungwa na Shamim Hamisi dakika ya 69 na Stumai Abdallah dakika ya 70.
  Kikosi cha Temeke kilikuwa; Belinda Julius, Ever Wailes/Fabiola German dk80+2, Ziada Ramadhani, Violeth Nicolas, Zuwena Aziz, Sada Ramadhani, Swaum Salum/Neema Ismail dk74, Shamin Hamisi, Hafidha Juma/Halima Hamdan dk40, Neema Paul na Stumai Abdalalah.
  Stumai Abdallah wa Temeke akimtoka beki wa Ilala
  Ziada Ramadhani wa Temeke akiwatoka mabeki wa Ilala
  Ilala; Hamisa Chande, Saraphina Peter/Maria Bayo dk27, Rose Mpoma, Khadija Ally, Mayciana Prosper, Batuli Mohammed, Zainab Mlenda/Jaqcueline Albert dk45, Hamida Fadhil, Fatuma Issa/Salma Masoud dk41, Madeline Sylvester/Aisha Kidunda dk66 na Ramla Said/Mariam Said dk41. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TEMEKE YAWASHUGHULIKIA KISAWASAWA ‘MASISTADUU’ WA ILALA KOMBE LA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top