• HABARI MPYA

  Saturday, January 31, 2015

  DOMAYO AFUNGA YOTE MAWILI AZAM IKITOA 2-2 NA ZESCO UNITED

  AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 ma ZESCO United ya Zambia katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa TP Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Frank Domayo, ingawa taarifa haikuwataja wafungaji wa mabao wa ZESCO, timu yenye mshambuliaji Mtanzania, Juma Luizio.
  Hiyo ni mechi ya pili katika ziara ya mabingwa hao wa Tanzania Bara mjini Lubumbashi, baada ya awali kufungwa 1-0 na wenyeji TP Mazembe Jumatano.
  Azam FC iliyokwenda huko kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan katikati ya mwezi ujao, itacheza mechi ya mwisho dhidi ya Don Bosco Jumanne.
  Katika mchezo wa kwanza leo, TP Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwwngu, iliwafunga Don Bosco mabao 3-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DOMAYO AFUNGA YOTE MAWILI AZAM IKITOA 2-2 NA ZESCO UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top