• HABARI MPYA

  Thursday, January 29, 2015

  FIFA WATUA DAR KUCHUNGUZA UPANGAJI MATOKEO

  Rais wa FIFA, Sepp Blatter akiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kulia
  UJUMBE wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) upo nchini kuchunguza tuhuma za upangaji matokeo.
  Waamuzi waliosimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na watu wengine watahojiwa na ujumbe huo. Matokeo ya uchunguzi huo yatatangazwa na FIFA baada ya shughuli hiyo kukamilika.
  “Tunaendelea kuwahimiza wanafamilia wa mpira wa miguu wazidi kuzingatia kanuni za maadili za TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na FIFA katika utendaji wao. FIFA itahakikisha kuwa haki inatendeka katika uchunguzi ambao inaufanya,”imesema taarifa ya TFF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA WATUA DAR KUCHUNGUZA UPANGAJI MATOKEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top