• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  DAKTARI: OKWI CHUPU CHUPU AFE

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  DAKTARI wa Simba SC, Yassin Gembe amesema mshambuliaji Emmanuel Okwi ameruhusiwa kutoka hospitali, lakini leo Mganda huyo amechungulia kifo.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu, Gembe amesema kwamba Okwi amerejea nyumbani baada ya matibabu katika hospitali ya Muhimbili, lakini alikumbana na mkasa mbaya maishani.
  “Okwi aligongwa kiwiko nyuma ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu, kwa hiyo akapoteza fahamu uwanjani. Ilikuwa mbaya sana, angeweza kupoteza maisha, lakini hali ile tuliidhibiti wakati tunampa huduma ya kwanza uwanjani,”.
  “Baada ya hapo, tukaingia naye ndani kwenye zahanati ndogo ya Uwanja, kuendelea kumpa tiba hadi fahamu zikamrejea, lakini hali yake haikuwa nzuri sana, ikabidi tumkimbize Muhimbili, ambako baada ya tiba ya takriban saa mbili, sasa yuko vizuri,”amesema Gembe.
  Hata hivyo, Gembe amesema mchezaji huyo hataendeelea na mazoezi kesho akiwa mapumzikoni, ili kupata nafuu zaidi. 
  Dk Yassin Gembe (kulia) amesema Okwi amechungulia kifo leo\
  Okwi baada ya kuzimia leo Uwanja wa Taifa
  Okwi aliifungia timu yake bao la kuongoza katika sare ya 1-1 na Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kuzimia kipindi cha pili kufuatia kugongana na beki Aggrey Morris wa Azam na kukimbizwa hospitali ya taifa, Muhimbili.
  Okwi alitibiwa kwa dakika 10 kwenye zahanati ndogo iliyopo ndani ya Uwanja wa Taifa, lakini hakupata nafuu akakimbizwa Muhimbili. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DAKTARI: OKWI CHUPU CHUPU AFE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top