• HABARI MPYA

  Saturday, January 24, 2015

  MAN CITY YATOLEWA NISHAI NA BORO, YAPIGWA 2-0 ETIHAD NA KUTUPWA NJE KOMBE LA FA

  MAKUBWA yametokea leo katika soka ya Uingerea. Mabingwa wa England, Manchester City wamechapwa mabao 2-0 na Middlesbrough katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA leo Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya timu hiyo ya Daraja la Kwanza, yamefungwa na Patrick Bamford anayecheza kwa mkopo kutoka Chelsea dakika ya 52 na Kike dakika ya 90.
  Boro sasa inakwenda Raundi ya tano michuano hiyo baada ya kuving’oa vigogo siku ya leo.
  Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Caballero, Zabaleta, Boyata, Kompany, Kolarov, Navas/Lampard dk67, Milner, Fernando/Dzeko dk79, Silva, Aguero na Jovetic/Fernandinho dk67.

  Middlesbrough; Mejias, Whitehead, Ayala, Gibson, Friend, Bamford, Clayton, Leadbitter, Adomah, Vossen/Kike dk87 na Tomlin/Reach dk81.
  Bamford (second right) celebrates with his team-mates after scoring at Etihad Stadium in the FA Cup fourth round
  Bamford (wa pili kulia) akishangilia na wenzake baada ya kufunga Uwanja wa Etihad leo
  Manchester City players James Milner (left), Dedryck Boyata (centre) and Fernando look dejected after their side concede
  Wachezaji wa Manchester City, James Milner (kushoto), Dedryck Boyata (katikati) na Fernando wakiwa hawaamini kilichotokea

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2924606/Manchester-City-0-2-Middlesbrough-Chelsea-loanee-Patrick-Bamford-Kike-strike-Boro-record-stunning-FA-Cup-win.html#ixzz3PlNii6RP 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YATOLEWA NISHAI NA BORO, YAPIGWA 2-0 ETIHAD NA KUTUPWA NJE KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top