• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  ARSENAL YAEPUKA BALAA LA CHELSEA NA MAN CITY, YAGONGA 'VITOTO' 3-2 KOMBE LA FA

  ARSENAL imeichapa Brighton mabao 3-2 katika mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA leo, siku moja baada ya vigogo Chelsea na Manchester kuadhiriwa na timu za Daraja la Kwanza.
  Theo Walcott aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya pili, kabla ya Mesut Ozil kufunga la pili dakika ya 24 akimalizia pasi safi ya Tomas Rosicky. 
  Chris O'Grady akaifungia bao la kwanza Brighton akitumia makosa ya beki Calum Chambers, lakini Rosicky restored akauimarisha ushindi wa Arsenal kwa bao la tatu baada ya gonga safi kati yake na Olivier Giroud.
  Sam Baldock akawafungia wenyeji bao la pili akimtungua vizuri Wojciech Szczesny dakika ya 75
  Kikosi cha Brighton kilikuwa; Stockdale, Saltor/March dk63, Greer, Dunk, Bennett, Calderon, Holla, Ince, Baldock, Forster-Caskey/Colunga dk81 na O'Grady.
  Arsenal: Szczesny, Chambers, Koscielny, Monreal, Gibbs, Flamini, Ramsey, Walcott/Sanchez dk69, Ozil/Coquelin dk79, Rosicky na Giroud/Akpom dk69.
  Ozil's goal was his first since returning from a serious knee injury sustained against Chelsea back in October last year
  Mesut Ozil ameifungia bao la kwanza Arsenal baada ya kurejea kutoka kwenye maumivu ya goti yaliyomuweka nje tangu Oktoba mwaka jana baada ya kuumia dhidi ya Chelsea

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2925657/Brighton-2-3-Arsenal-Theo-Walcott-Mesut-Ozil-Tomas-Rosicky-target-Gunners.html#ixzz3PrHPgDYF 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAEPUKA BALAA LA CHELSEA NA MAN CITY, YAGONGA 'VITOTO' 3-2 KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top