• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  KIGOMA YAITUPA NJE MWANZA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE, MCHEZAJI APASULIWA HADI DAMU CHAMAZI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIGOMA imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Taifa la wanawake, baada ya kuifunga mabao 2-1 Mwanza katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
  Shujaa wa Kigoma leo alikuwa ni mshambuliaji Jaqcueline Richard aliyefunga mabao yote hayo mawili kipindi cha pili, baada ya dakika 45 za kwanza kwisha bila mabao.
  Jaqcueline alifunga mabao hayo dakika za 56 na 71, wakati bao pekee la Mwanza lilifungwa na Veronica John dakika ya 66.  
  Jaqcueline Richard (katikati) akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Kigoma bao la ushindi katika Robo Fainali ya Kombe la Taifa la Wanawake leo
  Mshambuliaji wa Mwanza, Merian Kimbuya 'Mtumba' akimiliki mpira mbele ya beki wa Kigoma, Rehema Heri leo

  Katika mchezo huo, Mwanza ilipata pigo dakika ya 40 baada ya mchezaji wake, Wisala Julius kuchanika juu ya jicho la kushoto baada ya kugongana na mchezaji wa Kigoma.
  Wisala alitolewa nje akivuja damu na kwenda kutibiwa katika gari la wagonjwa lililokuwapo Uwanja wa Azam Complex leo.
  Kikosi cha Kigoma kilikuwa; Janet Shijja, Odria Gabriel, Vene Gedion, Neema Charles, Neema Sanga, Rehema Heri, Acavila Gaspary Jaqcueline Richard, Aziza Lugendo, Aisha Juma na Rahabu Joshua/Kitenge Nusura dk46.
  Mwanza; Anna Mathias, Samira Ally, Grace Dismas, Wisala Julius/Hamisa Athumani dk42, Salma Mpanja, Herrieth Edward, Nabila Ahmad Hazaa, Merian Kimbuya, Veronica John na Mwanamvua Seif.
  Herrieth Edward wa Mwanza (kushoto) akimdhibiti Veneranda Gedion wa Kigoma katika mchezo huo
  Wisala Julius akishonwa sehemu aliyochanika leo Chamazi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIGOMA YAITUPA NJE MWANZA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE, MCHEZAJI APASULIWA HADI DAMU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top