• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 30, 2015

  FRIENDS RANGERS YAPOTEZA MECHI KWA KUGOMA

  MECHI namba 120 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kundi A kati ya Majimaji na Friends Rangers iliyochezwa jana (Januari 29 mwaka huu) Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilivunjika dakika ya 38 baada ya Friends Rangers kugoma kuendelea na mchezo.
  Kwa kitendo hicho, Friends Rangers imepoteza mchezo huo. Hatua nyingine za kikanuni zitafuata baada ya kamati inayohusika kukutana.
  Wakati huo huo, mechi ya FDL kundi A iliyochezwa leo (Januari 30 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kati ya African Lyon na Ashanti United imemalizika kwa sare ya bao 1-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FRIENDS RANGERS YAPOTEZA MECHI KWA KUGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top