• HABARI MPYA

  Tuesday, January 27, 2015

  TEMEKE YAITUPA NJE MBEYA KOMBE LA TAIFA, SASA KUVAANA NA ILALA IJUMAA CHAMAZI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  TEMEKE imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake, baada ya kuitandika Mbeya mabao 3-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
  Kwa matokeo hayo, Temeke itakutana na mahasimu wao wakubwa, Ilala katika Nusu Fainali Ijumaa, Uwanja wa Azam Complex.
  Mabao ya Temeke leo yamefungwa na Stumai Abdallah mawili dakika za 28 na 40, wakati lingine limefungwa na Neema Paul dakika ya 72.
  Kwa ujumla, Temeke iliifunika Mbeya uwanjani leo na sasa wapenzi wa soka watarajie Nusu Fainali mbili kali, kati ya TMK na Ilala na Kigoma na Pwani Alhamisi. 
  Kikosi cha Temeke kilichoifunga 3-0 Mbeya leo Chamazi
  Ever Wailes akiweka mpira kifuani mbele ya winga wa Mbeya, Diana Msewa leo Chamazi

  Katika mchezo wa kwanza, Ilala iliifunga Iringa mabao 2-1. Mechi za leo zilihudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi. 
  Kikosi cha Temeke kilikuwa; Belinda Julius, Ever Wailes/Fabiola German dk80+2, Ziada Ramadhani, Violeth Nicolas, Zuwena Aziz, Sada Ramadhani, Swaum Salum/Neema Ismail dk74, Shamin Hamisi, Hafidha Juma/Halima Hamdan dk40, Neema Paul na Stumai Abdalalah.
  Mbeya: Nisa Kamala, Jasmin Chambua/Janeth Mapunda dk40, Magreth Charles/Neema Ambonisye dk24, Asteria Andrew, Bahati Mapunda/Hanifa Gramseni dk76, Lucy Adam, Saida Mkambala/Kapangala John dk66, Opper Clement, Mariam Yussuf, Happy Jeshi/Sunga Edson dk38 na Diana Msewa/Aida Anthony dk40.
  Nyota wa Temeke, Stumai Abdallah akipasua katikati ya wachezaji wa Mbeya

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TEMEKE YAITUPA NJE MBEYA KOMBE LA TAIFA, SASA KUVAANA NA ILALA IJUMAA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top