• HABARI MPYA

  Thursday, January 29, 2015

  SARAFU YAIPAMBANISHA GUINEA NA GHANA ROBO FAINALI AFCON, MALI SAFARI NYUMBANI

  TIMU ya Guinea imeipiku Mali na kutinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchezeshwa bahati nasibu katika zoezi lililofanyika mjini Malabo leo.
  Bahati nasibu iliamua mshindi wa pili wa Kundi D kufuatia timu zote kulingana kwa kila kitu baada ya mechi zao tatu za makundi. Ivory Coast iliyomaliza na pointi tano imeongoza Kundi.
  Sare tatu mfululizo za 1-1 kwa timu zote zilimaanisha haziwezi kutenganishwa kwa pointi, wala mabao na baada ya Guinea kufuzu kwa sarafu sasa itamenyana na Ghana Jumapili mjini Malabo.
  Mechi za Robo Fainali zinatarajiwa kuchezwa Jumamosi na Jumapili wiki hii, Kongo itamenyana na jirani zao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uwanja wa Bata na baadaye wenyeji, Equatorial Guinea watamenyana na Tunisia Jumamosi.
  Jumapili duru la Robo Fainali litafungwa kwa michezo kati ya Guinea na Ghana na Algeria na Ivory Coast Uwanja wa Malabo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SARAFU YAIPAMBANISHA GUINEA NA GHANA ROBO FAINALI AFCON, MALI SAFARI NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top