• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 30, 2015

  CHELSEA KUMKOSA DIEGO COSTA DHIDI YA MAN CITY KESHO, AFUNGIWA MECHI TATU NA FA

  KLABU ya Chelsea itamkosa mkali wake wa mabao Diego Costa kesho katika mechi ya kuwania usukani wa Ligi Kuu ya England, dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City baada ya kufungiwa mechi tatu na Chama cha Soka (FA).
  Mshambuliaji huyo Hispania alikutwa na hatia ya kumkanyaga makusudi mchezaji wa Liverpool, Emre Can katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup Uwanja wa Stamford Bridge mapema wiki hii.
  Costa alishitakiwa na FA Jumatano jioni na pamoja na utetezi wa Chelsea kwamba alikuwa haoni anapokanyaga mguu wake akamkanyaga kwa bahati mbaya Can, lakini ameadhibiwa.
  Diego Costa, training with Chelsea on Thursday, contested his FA charge for stamping on Emre Can
  Diego Costa, akiwa mazoezini na Chelsea jana, amefungiwa na FA kwa kumkanyaga Emre Can
  Chelsea striker Costa (right) moves towards the ball after Can takes a tumble off the pitch
  Mshambuliaji wa Chelsea, Costa (kulia) akiwahi mpira baada ya Can kuanguka uwanjaniCosta appears to stamp on Can's right leg during a feisty opening period at Stamford Bridge
  Costa alionekana akimkita Can katika mguu wa kulia Uwanja wa Stamford Bridge
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA KUMKOSA DIEGO COSTA DHIDI YA MAN CITY KESHO, AFUNGIWA MECHI TATU NA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top