• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  HABARI NJEMA THE GUNNERS, BEKI LA MAANA GABRIEL PAULISTA NJIANI KUTUA ARSENAL, KILA KITU SAFI

  KLABU ya Villarreal imethibitisha imekubaliana kimsingi na Arsenal biashara ya beki Gabriel Paulista kuhamia The Gunners kwa dau la Pauni Milioni 15.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye hivi karibuni kocha Arsene Wenger alithibitisha yupo kwenye rada zake, anatarajiwa kuhamia Arsenal, huku Joel Campbell akihamia timu hiyo ya La Liga kwa mkopo kumalizia msimu, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yao.  
  Habari zinakuja baada ya Paulista kuachwa katika kikosi cha wachezaji 18 wa Villarreal waliomenyana na Levante Uwanja wa El Madrigal jana usiku, hali ambayo inaongeza uwezekano wa Mbrazil huyo kutua Emirates.
  The Brazilian defender will be looking to bolster Arsenal's defensive ranks if a move goes through
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HABARI NJEMA THE GUNNERS, BEKI LA MAANA GABRIEL PAULISTA NJIANI KUTUA ARSENAL, KILA KITU SAFI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top