• HABARI MPYA

  Saturday, January 24, 2015

  PLUIJM ABADILI KIKOSI YANGA, TAMBWE NA MBUYU TWITE NJE, MRWANDA AANZA NA SHERMAN LEO DHIDI YA POLISI

  Na Mahmoud Zubeiry, MOROGORO
  KOCHA wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm leo amebadilisha safu yake ya ushambuliaji, akiwaanzisha Danny Mrwanda pamoja na Mliberia Kpah Sherman.
  Yanga SC itamenyana na Polisi ya hapa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri na sasa hivi vikosi vinapasha misuli moto uwanjani.
  Awali, Pluijm amekuwa akiwaanzisha pamoja Mrundi Amisi Tambwe na Sherman, lakini baada ya uhaba wa mabao katika mechi tatu zilizopita, leo amebadilisha mipango.
  Viungo wa pembeni leo wataendelea kuwa Simon Msuva na Mbrazil, Andrey Coutinho, wakati viungo wengine ni Salum Telela na Mnyarwanda Haruna Niyonzima.
  Kpah Sherman ameanza na Danny Mrwanda leo

  Safu ya ulinzi inaundwa na Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
  Katika benchi wapo, Deo Munishi ‘Dida’, Edward Charles, Rahab Zahir, Hassan Dilunga, Tambwe, Jerry Tegete na Hussein Javu. Wachezaji mashuhuri wa kikosi cha kwanza ambao hawapo kabisa leo ni beki Mbuyu Twite na mshambuliaji Mrisho Ngassa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM ABADILI KIKOSI YANGA, TAMBWE NA MBUYU TWITE NJE, MRWANDA AANZA NA SHERMAN LEO DHIDI YA POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top