• HABARI MPYA

    Tuesday, January 27, 2015

    MWANZA WAIKATIA RUFAA KIGOMA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE, KISA KUTUMIA MAMLUKI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    MWANZA wameikatia rufaa Kigoma baada ya kukiuka kanuni za michuano ya Kombe la Taifa la Wanawake kufuatia kutumia wachezaji wa timu ya taifa, na ambao wamekwishachezea timu nyingine kwenye michuano hiyo.
    Kigoma iliifunga mabao 2-1 Mwanza katika mchezo wa Robo Fainali uliofanyika jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, lakini kikosini inadaiwa ilikuwa ina ‘mamluki’.
    Nahodha wa Mwanza, Wanniyah Maulid ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, wachezaji wa timu ya taifa ambao Kigoma iliwatumia ni Aziza Lugendo, Neema Sanga, Jacqueline Richard mfungaji wa mabao yote mawili na Vene Gedion, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za mashindano.
    Wanniah amesema Mwanza wameka rufaa dhidi ya Kigoma

    Aidha, Wanniyah amesema kuna wachezaji ambao anawakumbuka walikutana nao katika hatua za awali za michuano hiyo wakichezea timu nyingine walizofanikiwa kuzitoa, lakini jana waliibukia kikosi cha Kigoma.
    Wanniyah, kiungo wa Mwanza ambaye hakucheza jana kwa sababu ya maumivu ya kifundo cha mguu yanayomsumbua kwa wiki ya pili sasa, amesema kwamba Mwenyekiti wa timu yao, Sophia Tigalyoma na Katibu wake, Hawa Bajanguo wamefuata taratibu zote kukata rufaa hiyo.
    “Tuna matumaini ya kurudishwa kwenye mashindano kwa sababu Kigoma wamekiuka kanuni za mashindano, hivyo hawastahili kuendelea,”alisema Wanniyah ambaye anaendelea na masomo katika sekondari ya Masaka, nchini Uganda.       
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANZA WAIKATIA RUFAA KIGOMA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE, KISA KUTUMIA MAMLUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top