• HABARI MPYA

  Thursday, January 29, 2015

  REFA WA 'SHY TOWN' ALIVYOPIGWA MKWARA NA MKUDE, MESSI HADI AKARUDISHA KADI NYEKUNDU MFUKONI

  Refa Abdallah Kambua wa Shinyanga (kulia) jana alitoa kadi nyekundu kwa ajili ya kumpa mchezaji mmoja wa Simba, lakini wachezaji wa timu hiyo walimvamia na kumuwekea mikwara, kumbembeleza hadi akairudisha mfukoni kadi hiyo. Pichani wachezaji wa Simba ni Ramadhani Singano 'Messi', Jonas Mkude na Abdi Banda anayeonekana kuwasihi wenzake waache kumzonga mwamuzi huyo.
  Tukio lilitokea baada ya kipa Peter Manyika (kulia) kumdaka miguu mchezaji wa Mbeya City, Raphael Daudi akiwa anakwenda kufunga, huvyo refa kupuliza filimbi ya kuamuru penalti.

  Hatimaye Kambua kutoka Shy Town akanywea na kuirudisha kadi nyekundu mfukoni, penalti ikapigwa Simba akafa 2-1. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA WA 'SHY TOWN' ALIVYOPIGWA MKWARA NA MKUDE, MESSI HADI AKARUDISHA KADI NYEKUNDU MFUKONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top