• HABARI MPYA

  Saturday, January 24, 2015

  RONALDO ALIMWA NYEKUNDU KWA ‘UBONDIA’, REAL MADRID YASHINDA 2-1 KWA MBINDE

  REAL Madrid imeshinda mabao 2-1 dhidi ya Cordoba katika La Liga, lakini mshambuliaji Cristiano Ronaldo amelimwa kadi nyekundu.
  Ronaldo alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 82 baada ya kumpiga ngumi Jose Angel Crespo.
  Nyota huyo wa Ureno na Mwanasoka Bora wa Dunia, sasa anakabiliwa na hatari ya kufungiwa mechi tatu.
  Nabil Ghilas aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya tatu kwa penalti baada ya beki wa Real, Sergio Ramos kuunawa mpira. Karim Benzema akasawazisha dakika ya saba akimalizia kazi ya Gareth Bale.Cristiano Ronaldo lashes out at Cordoba's Jose Angel Crespo as the frustration begins to boil over
  Cristiano Ronaldo akimpiga ngumi mchezaji wa Cordoba, Jose Angel Crespo 

  Bale akaifungia Real bao la ushindi kwa penalti akinufaika na kutokuwepo kwa Ronaldo uwanjani dakika ya 89. Nicolas Cartabia wa Cordoba pia alionyeshwa kadi nyekundu. 
  Kikosi cha Cordoba kilikuwa: Martin Corral, Gunino, Pantic, Crespo, Fraga, Rodríguez Barrera, Rossi, Bebe, Nicolas Cartabia, Ghilas, And one/Vico Villegas dk80.
  Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo/Fabio Coentrao dk72, Khedira/Illarramendi dk64, Kroos, Rodriguez/Jese dk80, Bale, Benzema na Ronaldo.
  Referee Alejandro Jose Hernandez Hernandez had little choice but to show Ronaldo a straight red card following the incidents
  Refa Alejandro Jose Hernandez hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Ronaldo 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2924614/Cordoba-1-2-Real-Madrid-Gareth-Bale-saves-Cristiano-Ronaldo-s-blushes-late-penalty-Porgtuguese-forward-sent-off.html#ixzz3PlXHUTOZ 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO ALIMWA NYEKUNDU KWA ‘UBONDIA’, REAL MADRID YASHINDA 2-1 KWA MBINDE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top