• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  PWANI YAWACHEZESHA MDUNDIKO TANGA, YAWATANDIKA 5-2 KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  PWANI imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Taifa Wanawake, baada ya kuifunga Tanga mabao 5-2 katika mchezo wa Robo Fainali uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, usiku huu.
  Mabao ya Pwani yamefungwa na Tumaini Michael  dakika ya saba, Johari Shaaban dakika ya 13, Jane Claude dakika ya 32, Mwanaidi Salum dakika ya 40 na Wema Richard dakika ya 47.
  Winga wa Pwani, Jane Cloudy (kushoto) akishangilia baada ya kuifungia Pwani bao la tatu leo
  Jane Cloude kushoto akimtoka beki wa Tanga, Mwanaiswha Mussa Seif 

  Tanga yenyewe ilipata mabao yake kupitia kwa Asha Shaaban Hamza dakika ya nane na Tatu Nuru Malogo dakika ya 17. Pwani sasa itamenyana na Kigoma iliyoitoa Mwanza kwa kuifunga mabao 2-1 katika mchezo uliotangulia jioni ya leo. 
  Kikosi cha Pwani kilikuwa; Gelewa Yona, Zaituni Iddy/Mwanaidi Salum, Shani Sultani, Anna Christopher, Wema Richard, Faidhia Athumani, Jane Cloude, Monica Henry/Arafa Yahya, Johari Shaaban/Jamila Kassim, Tumaini Michael na Amina Ramadhani.
  Tanga; Rene James Lekey, Mwanaisha Mussa Seif, Blandina Wenslaus Usiku, Mwanamvua Mohammed, Rukia Maulid Abeid/Happyness Charles, Christina Francis Pancras/May Raphael, Tatu Nuru Malogo, Irene George Mngumbili, Veronica Gabriel Mapunda, Asha Shaaban Hamza na Rebecca Donald Frank/Wanja Mohammed.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PWANI YAWACHEZESHA MDUNDIKO TANGA, YAWATANDIKA 5-2 KOMBE LA TAIFA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top