// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); COASTAL UNION WAIFUATA STAND UNITED KIBABE SHY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE COASTAL UNION WAIFUATA STAND UNITED KIBABE SHY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, January 22, 2015

    COASTAL UNION WAIFUATA STAND UNITED KIBABE SHY

    Na Samira Said, TANGA
    TIMU ya Coastal Union imeondoka mkoani Tanga jana alfajiri kuelekea Mkoani Shinyanga ikiwa na wachezaji 20, walimu wawili na viongozi wa timu hiyo tayari kwa kucheza mechi yao ya Ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Stand United itakayopigwa kwenye uwanja wa Kambarage mjini humo.
    Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa wiki endi hii ikiwa ni muendelezo wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo timu hiyo itaingia uwanjani hapo ikiwa na matumaini ya kuweza kufanya vema baada ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
    Msafara wa timu hiyo unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Coastal Union, Albert Peter ambaye alisema kuwa mara baada ya kuwasilia mkoani humo watafanya mazoezi madogo madogo kabla ya mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi wiki hii.
    Akizungumzia hali za wachezaji wa timu hiyo, Kocha Mkuu, Mkenya James Nandwa alisema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mechi hiyo ili kuweza kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi kuu.

    Alisema kuwa licha ya michuano hiyo kuwa na upinzani mkubwa lakini wao wamejithatiti vilivyo ili kuweza kucheza kwa umakini ambao utawawezesha kupata matokeo mazuri.
    “Mipango yetu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri hasa ukizingatia mechi zetu mbili zilizopita hatukufanya vizuri hivyo tutahakikisha tunapambana kufa na kupona kufanikisha lengo hilo muhimu kwetu “Alisema Kocha Nandwa.
    Hata hivyo aliwataka wapenzi na mashabiki wa soka mkoani Tanga wanaoishi mkoani Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenye mechi hiyo lengo likiwa kuwapa hasama wachezaji wa timu hiyo.
    Timu ya Coastal Union itaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupata sare kutokufungana nyumbani dhidi ya Polisi Morogoro ambapo hivi sasa ina pointi 13 ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi kuu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION WAIFUATA STAND UNITED KIBABE SHY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top