• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  FABIAN DELPH 'AWACHINJIA BAHARINI' LIVERPOOL, AONGEZA MKATABA ASTON VILLA

  KIUNGO Fabian Delph amezima tetesi za kuhamia Liverpool baada ya kusaini Mkataba mpya wa miaka minne na nusu na klabu yake, Aston Villa.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England imetangaza kumpa Mkataba mpya Delph Jumapili na kumzuia kuhamia Anfield.
  Liverpool iliripotiwa kumtaka Delph akawe mbadala wa Nahodha, Steven Gerrard lakini kocha Paul Lambert amechukua hatua za haraka kumtia pingu mchezaji huyo.
  Fabian Delph amejitia kitanza cha miaka minne na nusu zaidi Aston Villa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FABIAN DELPH 'AWACHINJIA BAHARINI' LIVERPOOL, AONGEZA MKATABA ASTON VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top