• HABARI MPYA

  Thursday, January 29, 2015

  MAMILIONI YA WAARAABU YATAMBA ULAYA, UWANJA WA REAL MADRID SASA KUITWA ABU DHABI BERNABEU

  HUKU tayari wakiwa wanatangaza maajina yao kupitia klabu moja kubwa barani Ulaya, Manchester City, Abu Dhabi sasa inataka kuweka jina ;ake katika Uwanja mkubwa dunani, Santiago Bernabeu.
  Kampuni hiyo ya Uarabuni, ikiwa inaimiliki Manchester City, ilijiingiza katika ushirika wa kibiashara na klabu ya Real Madrid Novemba mwaka jana, ikitoa Pauni Milioni 15 kwa mwaka ili kuweka jina lao kwenye Uwanja huo, kwa mujibu wa Diario AS.
  Coca-Cola na Microsoft wote walionyesha nia ya kuweka majina yao kwenye Uwanja wa Bernabeu, lakini inaoneekana kama kampuni ya Cepsa ya Hispania, ambayo inamilikiwa na IPIC (Kampuni ya Uwekezaji wa Kimataifa kwenye Petroli) ambayo nayo inamilikiwa na serikali ya Abu Dhabi, ndiyo itashinda bafasi hiyo. 
  Real Madrid's Santiago Bernabeu stadium is set to be renamed Abu Dhabi Bernabeu
  Uwanja wa Real Madrid, Santiago Bernabeu ambao unaweza kubadilishwa jina na kuwa Abu Dhabi Bernabeu
  The Bernabeu was opened in 1947 and is one of the most iconic venues in world football
  Uwanja wa Bernabeu ulifunguliwa mwaka 1947 na moja ya viwanja vikubwa duniani

  WASIFU WA UWANJA WA REAL MADRID

  Jina: Santiago Bernabeu
  Ukubwa: Kungiza watu 81,044
  Kujengwa: 1944 hadi 1947
  Kufunguliwa: 1947
  Mechi ya kwanza: Real Madrid 3-1 OS Belenenses
  Uwanja huo ulipewa jina la Mwenyekiti wa zamani wa Real, Santiago Bernabeu Yeste.
  Kampuni ya Cepsa yenye maskani yake mjini Madrid, ni ya nne kwa ukubwa katika viwanda vya Hispania, wakati  IPIC, iliyoundwa mwaka 1984, imewekeza kwenye makampuni makubwa 18 yanayoongoza ikiwa na nguvu kubwa duniani. 
  Mwezi Novemba mwaka jana IPIC na Real zilitangaza ndoa yao, kupitia kwa Rais wa Madrid, Florentino Perez ambaye alinaswa na picha za kamera akisema Uwanja utatiwa ‘IPIC ay Cespa, vyovyote watakavyotaka.
  Kwa mujibu wa taarifa za AS, wadhamini wanataka kuweka jina la ‘Abu Dhabi Bernabeu’. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMILIONI YA WAARAABU YATAMBA ULAYA, UWANJA WA REAL MADRID SASA KUITWA ABU DHABI BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top