• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 29, 2015

  BARCA YATINGA NUSU KOMBE LA MFALME, YAICHAPA 2-1 ATLETICO MADRID

  BARCELONA imetinga Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme, Hipsania ikijulikana kama Copa del Rey  baada ya kuilaza mabao 3-2 Atletico Madrid, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla 4-2.
  Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Fernando Torres aliifungia Atletico sekunde ya 39, kabla ya Barcelona kusawazisha dakika ya tisa.
  Luis Suarez akamsetia Mbrazil, Neymar kuifungia bao la pili Barca, kabla ya Raul Garcia kuisawazishia Atletico Madrid dakika ya 11.
  Miranda akajifunga kuipatia bao Barca bao la tatu, kabla ya Gabi kutolewa kwa kadi nyekundu.
  Kikosi cha Atletico Madrid; Oblak, Juanfran/Gamez, dk58), Gimenez de Vargas, Miranda, Siqueira; Raul Garcia, Gabi, Suárez, Turan/Cani, dk63), Griezmann/Níguez, dk45 na Torres.
  Barcelona; Ter Stegen, Dani Alves, Pique, Mascherano/Mathieu dk61, Alba, Rakitic, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Neymar/Pedro, 77.
  Neymar silences the Vicente Calderon after firing Barcelona 3-2 up on the night against Atletico Madrid in the Copa del Rey
  Neymar akishangilia Uwanja wa Vicente Calderon baada ya kuiungia mabao maili katika ushindi wa 3- na Atletico Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCA YATINGA NUSU KOMBE LA MFALME, YAICHAPA 2-1 ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top