// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BAFANA BAFANA YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFCON, SENEGAL YANUSA 16 BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BAFANA BAFANA YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFCON, SENEGAL YANUSA 16 BORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, January 24, 2015

    BAFANA BAFANA YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFCON, SENEGAL YANUSA 16 BORA

    TIMU ya taifa ya Afrika Kusini imejiweka mguu nje kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea Eguatorial Guinea baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Senegal usiku huu Uwanja wa Mongomo.
    Oupa Manyisa alikaribia kuwa shujaa wa Bafana Bafana baada ya kufunga bao la kuongoxa dakika moja baada ya mapumziko, lakini Kara Mbodji akawasawazishia Simba wa Teranga dakika ya 60.
    Sare hiyo inaifanya Bafana Bafana iwe na pointi moja baada ya mechi mbili, kufutaia kufungwa mchezo wa kwanza na Algeria na sasa watalazimika kuifunga Ghana katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C kuangalia uwezekano wa kuingia 16 Bora.
    Mapema katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo Ijumaa, Ghana ilishinda 1-0 dhidi ya Algeria, shukrani kwake mfungaji wa bao hilo, Asamoah Gyan. Senegal inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, wakati Algeria na Ghana kila moja ina pointi tatu, wakati Bafana inashika mkia kwa pointi yake moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAFANA BAFANA YACHUNGULIA MLANGO WA KUTOKEA AFCON, SENEGAL YANUSA 16 BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top