• HABARI MPYA

  Thursday, January 22, 2015

  KIUNGO WA CHELSEA ATUA KWA MKOPO READING

  KIUNGO kinda anayepewa thamani ya juu wa Chelsea, Nathaniel Chalobah amejiunga na klabu ya Daraja la Kwanza, Reading inayosuasua kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu.
  Reading inashika nafasi ya 18 katika ligi, lakini kocha Steve Clarke anafahamu zaidi kuhusu uwezo wa Chalobah, kwa sababu alikuwa msaidizi wa Jose Mourinho mara ya kwanza Mreno huyo alipokuwa anafanya kazi Stamford Bridge.
  Mwanasoka huyo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya England, pia anaweza kucheza nafasi za ulinzi na Clarke anaamini Chalobah anaweza kuisaidia  The Royals kuepuka kushuka daraja.
  Nathaniel Chalobah poses with the number 14 shirt that he will wear while he is on loan at Reading
  Nathaniel Chalobah akiwa na jezi namba 14 ya Reading baada ya kujiunga nayo kwa mkopo kutoka Chelsea
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO WA CHELSEA ATUA KWA MKOPO READING Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top