• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  MASHABIKI SHINYANGA WAWATOLEA UVIVU VIONGOZI STAND UNITED

  Na Peter Andrew, SHINYANGA
  MASHABIKI wa timu ya soka ya Stand United ya Shinyanga, wameamua kuvunja ukimya na kuamua kuwatupia lawama viongozi wa timu hiyo kwa kushindwa kufanya vizuri uwanja wa nyumbani wa CCM Kambarage katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.
  Malalamiko hayo wameyatoa juzi wakati timu hiyo ilipokuwa na Coastal Union ya Tanga katika uwanja huo na wenyeji hao kupoteza kwa 1-0 lililofungwa na Godfrey Wambura dakika 46.
  Mashabiki hao Said Ally, Rushina Kashinje na Said Nassoro, walisema hawakubaliani na uongozi wa Stand United hasa kocha Emmanuel Masawe, kwa kushindwa kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo hasa katika uwanja wa nyumbani.
  Mashabiki mkoani Shinyanga baada ya Stand United kufungwa na Coastal Union jana

  “Hatuoni umuhimu wa Stand United kucheza nyumbani, kila tunapocheza tumekuwa watu wa kufungwa tu…viongozi gani hawana wasiotufaa na kocha anashindwa kutumia mbinu za ushindi ili timu iibuke na ushindi,” alisema Kashinje.
  Alisema timu nyingi zinazioshiriki Ligi Kuu Bara, zinapotumia viwanja vya nyumbani huvitumia vizuri kwa kupata ushindi lakini si kwa timu ya Stand United ambayo inagawa pointi na kuwaumiza mashabiki wake.
  Hata hivyo, mashabiki hao walitaja mechi ambazo Stand walicheza nyumbani na kuambulia kichapo ni dhidi ya Ndanda FC 4-1, Yanga 3-0, Azam 1-0 na Coastal Union 1-0.
  Mashabiki hao walisema katika mchezo wa juzi, walipanga kutembeza mkong’oto kuanzia kwa viongozi na kocha, lakini uwepo wa polisi kulisababisha kutofanya maamuzi hayo.
  Kocha msaidizi wa timu hiyo, Emmanuel Masawe, alisema timu yao imekosa umakini wa kushindwa kutumia nafasi wanazozipata na hivyo kusababisha kupokea kichapo toka kwa Coastal Union.
  Katika msimamo wa ligi kuu, Stand United imejikusanyia pointi 11 ikiwa inashikilia nafasi ya 13 juu ya Prisons yenye ponti 9.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHABIKI SHINYANGA WAWATOLEA UVIVU VIONGOZI STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top