• HABARI MPYA

  Thursday, January 29, 2015

  WAGANDA KUIPA YANGA SC MAKALI YA KUWAANGAMIZA WABOTSWANA, MKWASA APAA GABORONE KWENDA KUWATATHMINI WAPINZANI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itakwenda kuweka kambi visiwa vya Pemba na Unguja, Zanzibar kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya BDF XI ya Botswana, lakini pia itacheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi Vipers FC ya Uganda, zamani Bunamwaya.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, hawajajua mchezo na Vipers utafanyika wapi, kati ya Uganda na Tanzania, lakini utakuwapo.
  “Wale wana ratiba ya Ligi yao kule, sasa itategemea, tunaweza sisi tukawafuata kule, au wao wakaja. Ila kama watakuja, hiyo mechi itafanyika Zanzibar,”amesema Muro.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameelezea mkakati wa maandalizi ya klabu yake kwa mechi na BDF

  Kuhusu kambi, Muro amesema kwamba wataweka kambi ya kwanza Pemba, na baadaye watakwenda kumalizia Unguja, lengo pamoja na maandalizi mazuri, lakini pia kuwapa fursa wanachama wao wa kule, wawe na timu.
  Aidha, Muro amesema kwamba wapo kwenye mawasiliano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuomba mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopangwa kufanyika Februari 8, uahirishwe ili kupata fursa nzuri ya maandalizi ya mechi hiyo ya Afrika.
  Yanga SC inatarajiwa kumenyana na BDF kati ya Februari 13 na 15, mwaka huu katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam na marudano wiki inayofuata mjini Gaborone.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAGANDA KUIPA YANGA SC MAKALI YA KUWAANGAMIZA WABOTSWANA, MKWASA APAA GABORONE KWENDA KUWATATHMINI WAPINZANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top