• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 26, 2015

  ZAMBIA NJE, DRC NA TUNISIA ZAENDA ROBO FAINALI AFCON

  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika usiku wa leo, baada ya sare ya kufungana bao 1-1 na Tunisia katika mchezo wa Kundi B.
  Katika michuano hiyo inayoendelea nchini Equatorial Guinea, mchezo mwingine wa kundi hilo Cape Verde imetoka 0-0 na Zambia na zote zinaaga mashindano.
  Jeremy Bokila aliifungia bao la kusawazisha DRC dakika ya 66 baada ya Ahmed Akaichi kutangulia kuifungia Tunisia dakika ya 31. Tunisia imefuzu kama kinara wa Kundi hilo, kwa pointi zake tano, wakati DRC imefuzu kama mshindi pili kwa pointi zake tatu.
  Mapema jana, wenyeji Equatorial Guinea waliungana na Kongo kufuzu Robo Fainali za michuano hiyo kutoka Kundi A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZAMBIA NJE, DRC NA TUNISIA ZAENDA ROBO FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top