• HABARI MPYA

  Friday, January 23, 2015

  TIMU YA BEACH SOCCER ZANZBAR YAWASILI DAR

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  TIMU ya beach soccer ya Zanzibar imewasili Dar es Salaam leo mchana, tayari kwa kambi ya pamoja na Tanzania Bara kwa ajili ya kuunda kikosi cha Tanzania kitakashiriki mechi za mchujo za michuano ya Afrika.
  Tanzania imepangwa kucheza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayofanyika kati ya Februari 13 na 15 mwaka huu jijini Mombasa. Mechi ya marudiano itachezwa wiki moja baadaye nchini.
  Zanzibar imewasili na kikosi cha wachezaji 14 na viongozi watatu ambacho kitaungana na kile cha Tanzania Bara. Timu hizo zitacheza jumla ya mechi nane kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, Dar es Salaam.
  Mechi hizo zitachezwa mbili asubuhi na mbili jioni kesho (Januari 24 mwaka huu), na nyingine nne kwa utaratibu huo huo keshokutwa (Januari 25 mwaka huu) kabla ya Kocha John Mwansasu kutaja kikosi cha mwisho Januari 26 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA BEACH SOCCER ZANZBAR YAWASILI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top