• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 26, 2015

  FRIENDS RANGERS YAFUFUA MATUMAINI YA LIGI KUU, AFRICAN SPORTS YAIKALISHA MAJIMAJI

  BAO pekee la Ramadhani Hamidu dakika ya 20, limeipa ushindi wa 1-0 African Sports ya Tanga dhidi ya Majimaji, Uwanja wa Mkwakwani, mjini hapa katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
  Ushindi huo, unaifanya Sports ‘Wana Kimanumanu’, itimize pointi 41 baada ya kucheza mechi 19, ikiendelea kuwa kileleni mwa Kundi A, ikifuatiwa na Majimaji yenye pointi 36 za mechi 19 pia.
  Friends Rangers imeifunga Kurugenzi 2-0 na kufikisha pointi 35 katika nafasi ya tatu, baada ya mechi 19 pia, hivyo itakwenda kumenyana na Majimaji mwishoni mwa wiki, katika mchezo wa kuwania nafasi ya pili ya kupanda Ligi Kuu kutoka kundi hilo.

  Lipuli ya Iringa yenye pointi 35 pia za mechi 19, ni timu nyingine yenye nafasi ya kupanda Ligi Kuu kutoka Kundi A.
  Katika Kundi B, Toto African ya Mwanza ipo kileleni kwa pointi zake 39 za mechi 19, ikifuatiwa na Mwadui ya Shinyanga pointi 37 na JKT Oljoro ya Arusha pointi 32 za mechi 18.
  Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitapanda Ligi Kuu msimu ujao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FRIENDS RANGERS YAFUFUA MATUMAINI YA LIGI KUU, AFRICAN SPORTS YAIKALISHA MAJIMAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top