• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  OSCAR JOSHUA ASEMA REFA HAKUMTENDEA HAKI JUZI MOROGORO

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  BEKI wa kushoto wa Yanga SC, Oscar Joshua amesema kwamba refa Ahmada Simba wa Kagera alimpa kadi ya njano bila kosa juzi, timu ya ikimenyana na wenyeji Polisi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. 
  Yanga SC ilishinda 1-0 dhidi ya Polisi Jumamosi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, bao pekee la Dan Mrwanda na Oscar Joshua alionyeshwa kadi ya njano wakati anakwenda kurusha mpira.
  Beki hodari wa Yanga SC, Oscar Joshua kulia akimdhibiti kiungo msumbufu wa Polisi, Suleiman Kassim 'Selembe'  

  “Siku zote mimi huwa sipendi kubishana na marefa, nilikubali yaishe. Lakini alinionea tu,”alisema Oscar na kuongeza; “Mimi nimefika pale namuomba mtoto (muokota mipira) anipe mpira, yeye kazubaa, refa anakuja ananipa kadi,”.
  Oscar amesema kwamba anasahau hayo yote na anaelekeza fikra zake katika mchezo ujao wa timu yake, dhidi ya Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili washinde na kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OSCAR JOSHUA ASEMA REFA HAKUMTENDEA HAKI JUZI MOROGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top