• HABARI MPYA

  Thursday, January 22, 2015

  MARALIA YAWALAZA WAWILI NDANDA, KIKOSI CHAWEKA KAMBI SHINYANGA KUWAWINDA KAGERA SUGAR

  Na Juma Mohammed, MTWARA
  BAADA ya kupoteza mchezo wake na Simba SC katika uwanja wa nyumbani, Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0, timu ya Ndanda FC imetua Shinyanga jana kuweka kambi fupi kujiandaa na mchezo wao wa wikiendi dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
  Hata hivyo, timu hiyo imekumbwa na kadhia baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa wachezaji wake wawili kuugua Maralia. Ofisa Habari wa Ndanda FC, Idrisa Bandari amekiri kuwepo kwa wachezaji wanaoumwa huku akidai kuwa mbali na kupata kadhia hiyo maandalizi kuelekea mchezo wa Jumamosi yanaendela vizuri.

  ''Ni kweli wachezaji wetu wawili wanaumwa, lakini kama unavyojua timu ina wachezaji wengi kwa hiyo wakati hawa wakiendelea na matibabu maandalizi yataendelea kufanyika ili tuhakikishe tunapata ushindi,”alisema Bandari.
  Akizungumzia wamejipangaje kuhakikisha wanashinda mchezo wa ugenini ambao unatarajiwa kuwa mgumu, alisema kabla ya kwenda Mwanza watatafanya mazoezi Shinyanga lakini akasisitiza kuwa hawatacheza mechi yoyote ya kirafiki wakiwa hapo.
  ''Kwa sasa tunajiandaa kwa mazoezi tu hatuna programu ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu yoyote hapa Shinyanga''
  Timu ya Ndanda imepoteza imani kwa mashabiki wake baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa mechi mbili mfululizo baada ya kutoka sare na Polisi Moro na kufungwa na Simba, hivyo mechi na Kagera Sugar ni muhimu kushinda kwao ili warudishe imani kwa mashabiki wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARALIA YAWALAZA WAWILI NDANDA, KIKOSI CHAWEKA KAMBI SHINYANGA KUWAWINDA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top