• HABARI MPYA

  Sunday, January 25, 2015

  BAHANUZI: NITARUDISHA HESHIMA YANGU TU

  Na Mahmoud Zubeiry, MOROGORO
  MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Said Rashid Bahanuzi anayecheza kwa mkopo Polisi Moro, amesema anaamini atarudisha kiwango chake na kuheshimika tena katika soka ya Tanzania.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu zake hizo, Bahanuzi alisema kwamba hajakata tamaa.
  “Umri bado unaniruhusu, na kwa kuwa huwa hapa (Polisi) walimu wananiamini na kunipa nafasi, basi nami nitatumia fursa hii kuinua tena kiwango changu,”alisema.
  Said Bahanuzi kushoto akiwatoka mabeki wa Yanga jana

  Yanga SC iliifunga Polisi bao 1-0 katika mchezo wa Kuu jana Uwanja wa Jamhuri na Bahanuzi alicheza dhidi ya timu yake hiyo ya Jangwani.    
  Shukrani kwake, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Davis Mrwanda aliyefunga bao hilo dakika ya 42 akimalizia mpira uliorudi baada ya kipa Tony Kavishe kupangua krosi ya Simon Msuva.
  Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa Sherman ambaye aliangushwa nje kidogo ya boksi na Haruna Niyonzima akaenda kumuanzia haraka Simon Msuva aliyemtoka beki Fanuel Simon na kutia krosi ya bao lililofungwa na Mrwanda, aliyesajiliwa Desemba Yanga SC kutoka Polisi.
  Bahanuzi aliingia kipindi cha pili na kuibadilisha kabisa Polisi, hadi ikaanza kulitia misukosuko lango la Yanga SC, kiasi kocha Pluijm kurekebisha ukuta wake, akimtoa Kevin Yondan na kumuingiza Rajab Zahir.
  Bahanuzi alikuwa mwiba kwa ukuta wa Yanga SC wakati wote kipindi cha pili na mara mbili alikaribia kufunga.
  Yanga SC iliamua kumtoa kwa mkopo Bahanuzi Polisi Moro, ilia pate nafasi ya kuchez na kuinua kiwango chake baada ya kuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya Jangwani. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAHANUZI: NITARUDISHA HESHIMA YANGU TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top