• HABARI MPYA

  Tuesday, January 27, 2015

  GHANA YATIGA ROBO FAINALI AFCON

  MABAO ya kipindi cha pili ya John Boye na Andre Ayew (pichani juu) yameipa Ghana ushindi wa 2-1 dhidi ya Afrika Kusini wakitoka nyuma kwa 1-0 Uwanja wa Mongomo na kutinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika usiku huu.
  Matokeo hayo, pamoja na ushindi wa 2-0 wa Algeria dhidi ya Senegal katika mchezo mwingine wa Kundi C, yanaifanya Ghana imalize kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake sita. 
  Algeria imemaliza nafasi ya pili, wakiwa na pointi sita pia, wakati Senegal imemaliza nafasi ya tatu na pointi zake nne na Afrika Kusini iliyoshika mkia imemaliza na pointi moja.
  Afrik Kusini; Brilliant Khuzwayo, Thabo Matlaba, Erick Mathoho, Anele Ngcongca, Rivaldo Coetzee, Thuso Phala/Sibusiso Vilakazi 58, Dean Furman, Andile Jali, Mandla Masango, Bongani Ndulula/Bernard Parker dk85, Tokelo Rantie/Reneilwe Letsholonyane 74.
  Kikoi cha Ghana kilikuwa, Razak Braimah, Harrison Afful, Daniel Amartey/John Boye dk36, Baba Rahman, Jonathan Mensah, Mubarak Wakaso, Afriyie Acquah/Emmanuel Agyemang-Badu dk70, Christian Atsu, Andre Ayew, Asamoah Gyan, Jordan Ayew/Kwesi Appiahdk sk71.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GHANA YATIGA ROBO FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top