• HABARI MPYA

  Monday, January 26, 2015

  WENYEJI EQUATORIAL GUINEA, KONGO WASONGA MBELE AFCON, BURKINA NA GUINEA WA KWANZA KUAGA MICHUANO

  MABAO ya Javier Balboa (pichani juu) na Ivan Salvador yamewahakikishia wenyeji, Equatorial Guinea kutinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Gabon katika mchezo wa Kundi A mjini Bata usiku wa Jumapili.
  Balboa alifunga kwa penalti dakika ya 55 kabla ya Slavador aliyetokea benchi kufunga la pili dakika ya 86. 
  Mchezo mwingine wa kundi hilo, Kongo imeifunga Burkina Faso mabao 2-1, maana yake inaungana na Equatorial Guinea kutinga hatua ya pili ya michuano hiyo.
  Kikosi cha Gabon kilikuwa: Ovono, Palun, Ondele, Ecuele Manga, Obiang/Lengoualama dk83, Madinda, Biyogho Poko/Ndong dk68, Kanga/Romaric dk77, Bulot, Aubameyang na Evouna
  Equatorial Guinea: Ovono, Randy, Da Gracia, Evuy, Sipo, Kike/Ivan Salvador dk67, Zarandona/Owona dk74, Ellong, Ivan, Balboa na Nsue/Ruben Dario dk89.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENYEJI EQUATORIAL GUINEA, KONGO WASONGA MBELE AFCON, BURKINA NA GUINEA WA KWANZA KUAGA MICHUANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top