• HABARI MPYA

  Saturday, January 31, 2015

  DRC YATANGULIA NUSU FAINALI AFCON, YAIFUMUA 4-2 KONGO

  JAMHURI ya KIdemokrasia ya Kongo (DRC) imetoka nyuma na kushinda 4-2 dhidi ya jirani zao, Kongo-Brazzaville mjini Bata, Equatorial Guinea hivyo kutinga Nusu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
  Mabao mawili ya Dieudonne Mbokani yametosha kuwafanya Chui hao watinge Nusu Fainali kwa mara ya kwanza tangu 1998.
  DRC sasa inasubiri  mshindi wa mechi ya Jumapili kati ya Ivory Coast na Algeria ikutane naye katika Nusu Fainali Februari 4.

  Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila bao leo, kabla ya mvua ya mabao kuanza kipindi cha pili, Dore February akiifungia bao la kwanza Kongo dakika ya 55 na Thievy Bifouma kufunga la pili dakika sita baadaye.
  DRC ilipata bao lake la kwanza dakika ya 65, mfungaji Mbokani kabla ya dakika 10 baaaye Jeremy Bokila kusawazisha.
  Joel Kimwaki akafunga bao la tatu dakika ya 80 kabla ya Mafoumbi kufunga la nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DRC YATANGULIA NUSU FAINALI AFCON, YAIFUMUA 4-2 KONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top