• HABARI MPYA

  Wednesday, January 28, 2015

  BEKI SIMBA SC AMKANA MKONGWE WA YANGA SI BABA YAKE

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Simba SC, Hassan Suleiman Isihaka ‘Mwana Dar es Salaam’ amesema hana uhusiano wowote wa kindugu na beki wa zamani wa Yanga SC, Isihaka Hassan ‘Chukwu’.
  Beki huyo chipukizi wa kati wa Wekundu wa Msimbazi anainukia vizuri katika klabu yake na soka ya Tanzania kwa ujumla kiasi cha kuanza kuteka hisia za wapenzi wa mchezo.
  Kutokana na majina yake kufanana na beki mwingine mahiri wa kati kuwahi kutoka nchini, Isihaka Hassan aliyewika miaka ya 1980, watu wakataka kujua undani wao.
  Nahodha wa Simba SC, Hassan Isihaka 'Mwana Dar es Salaam' amesema hana uhusiano na Isihaka Hassan 'Chukwu'

  Lakini BIN ZUBEIRY ilipofanya mahojiano na mchezaji huyo mwenye asili ya Kingazija jana, alisema; “Simjui huyu mtu, namsikia tu,”.
  “Na wala sina undugu naye, mimi baba yangu ni Suleiman Isihaka,”aliongeza baada ya kuulizwa kama ana udugu na beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
  Akiwa anajishindia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC kwa mara ya kwanza tangu apandishwe kutoka timu ya vijana ya Simba SC, maarufu kama Simba B, beki huyo ametokea kukubalika kwa kiasi kikubwa.
  Kocha wa sasa wa Wekundu wa Msimbazi, Mserbia Goran Kopunovic amempa beji ya Unahodha wa timu kinda huyo na anaitendea haki akiiongoza vyema safu ya ulinzi na timu kwa ujumla.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI SIMBA SC AMKANA MKONGWE WA YANGA SI BABA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top