• HABARI MPYA

  Friday, January 30, 2015

  SERIKALI YAAPA KUISHIKA KWA MIKONO MIWILI KILI MARATHON

  Na Mwandishi Wetu, MOSHI
  SERIKALI mkoani Kilimanjaro imesema itaendelea kuunga mkono mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon, kutokana na umuhimu wake kwa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
  Hakikisho hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa huo Severine Kahitwa, wakati wa uzinduzi wa maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka wa 2015, uliofanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro, juzi.
  “Mbali na kuinua kiwango cha michezo mkoani Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla, mashindano haya pias ni chachu katika kukua kwa uchumi wa Mkoa”, alisema.

  Mgeni rasimi katika hafla ya uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro marathoni katibu tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Severene Kahitwa akinyanyuwa bendera yenye nembo ya  Kilimanjaro Marathon kuashiria uzinduzi wa mbio hizo zitakazo fanyika Machi 1 mwaka huu,kushoto kwake ni Meneja wa bia ya Kilmanjaro Premium Lager Pamela Kikuli na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini David Charles pamoja na wadhamni shirikishi.

  Alisema mbali na kushiriki mbio hizo, washiriki kutoka zaidi ya nchi 40 hutembelea mbuga za wanyama na hivyo kuitangaza Tanzania haswa vivutio vyake vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro.
  “Utalii ni biashara kupbwa hapa Kilimanjaro na tukio hili limesaidia sana kuongeza biashara mkoani hapa kutokana na washiriki wengi wanaokuja kushiriki mbio hizi kukuza biashara zetu”, alisema.
  Mkuu huyo wa Mkoa alitoa shukrani zake za dhati na zile za uongozi wa Mkoa huo kwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo Kilimanjaro Premium Lager na kusema udhamini huo umekuwa pia ni chachu ya maendeleo ya michezo mkoani Kilimanjaro.
  Kwa upande wake, meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema kampuni yake itaendelea kuyadhamini mashindano hayo kazi ambayo wamekuwa wakiifanya tangu mashindano hayo yaanzishwe mwaka 2003. 
  Kilimanjaro Premium Lager jumla ya shilingi milioni 20 kama zawadi kwa washindi wa mbio ndefu za kilomita 42 ambapo washindi wa kwanza hadi wa tatu wanawake kwa wanaume watapata zawadi za shilingi milioni nne, milioni mbili na milioni moja. “Tunaamini kuwa zawadi hzi kuwa zawadi hizi zitatoa hamasa kwa wanariadha kujtuma zaidi waweze kuvunja rekodi mwaka huu”.
  Akitangaza udhamini wa Tigo kwa mbio hizo, Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini wa Tigo, David Charles alisema Tigo imetoa udhamini wa sh milioni 80 kwa mbio za kilomita 21 ambazo zitajulikana kama Tigo Kili Half Marathon na kuwa udhamini huo  ni sehemu ya wajibu wa kampuni hiyo katika maendeleo ya michezo nchini”.  
  Mbio hizi zinadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Tigo (Nusu Marathon), GAPCO (Mbio yaWalemavu), pamoja na wadhamini wa vituo vya maji kwenye mbio hizo ambao ni Kilimanjaro Water, FNB Tanzania, CMC Automobiles, Simba Cement, TPC Sugar, KK Security, Kibo Palace, Rwandair na UNFPA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAAPA KUISHIKA KWA MIKONO MIWILI KILI MARATHON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top