• HABARI MPYA

  Wednesday, January 28, 2015

  MAYWEATHER AMUIBUKIA PAQCUIAO USO KWA USO MIAMI, HALAFU...

  NYOTA wenye majina makubwa mchezo wa ngumi za kulipwa, Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wamejisogeza karibu na pambano lao, baada ya kukutana kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa mpira wa kikapu mjini Miami Marekani.
  Baada ya kukutana, wakali hao wa 'ndonga' wamekubaliana kuanza mipango ya pambano hilo lenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani Milioni 300. 
  Mayweather ndiye aliyenyanyuka na kumfuata Pacquiao wakati wa mapumziko katika mchezo wa kikapu kati ya Miami Heat dhidi ya Milwaukee Bucks na wawili hao wakapeana mikono, wakazungumza kwa muda mfupi, kisha wakabadilishana namba za simu.
  Pacquiao alisema: "Amenipa namba yake na amesema tutawasiliana,". Mtumiaji wa akaunti ya Twitter, Grant Smith ameposti picha kibao katika akaunti yake, @StrategySmith, wawili hao wakiwa wamesimama pamoja.
  These pictures posted on Twitter show Manny Pacquiao (left) and Floyd Mayweather meeting in Miami
  Picha hizi zimepostiwa kwenye akaunti ya Twitter zikiwaonyesha Manny Pacquiao (kushoto) na Floyd wakizungumza na kubadilishana namba za simu walipokutana mjini Miami

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/article-2929269/Coming-2015-Floyd-Mayweather-Manny-Pacquiao-attend-NBA-match-Miami-fueling-speculation-mega-fight.html#ixzz3Q7ItV6BD 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYWEATHER AMUIBUKIA PAQCUIAO USO KWA USO MIAMI, HALAFU... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top