• HABARI MPYA

  Saturday, January 24, 2015

  CHELSEA, MOURINHO WAUMBULIWA NA ‘KITIMU CHA MCHANGANI’, WAPIGWA 4-2 DARAJANI KWAO

  UNAANZAJE kuripoti kilichotokea Uwanja wa Stamford Bridge joni ya leo? Amini, usiamini.
  Kocha maneno mengi, Jose Mourinho wa Chelsea, Jose Mourinho alikuwa mdogo kama ‘piliton’ baada ya timu yake kufungwa mabao 4-2 na timu ha Daraja la Kwanza, Bradford City katika mchezo wa kwanza Raundi ya Nne Kombe la FA Uwanja wa Stamford Bridge, London.  
  Gary Cahill na Ramires waliifungia Chelsea na kuifanya iongoze 2-0 hadi dakika ya 38, lakini Bradford ikazinduka na kupata mabao manne kupitia kwa Jon Stead, Felipe Morais, Andy Halliday na Mark Yeates na kushinda mechi ugenini.
  Mshambuliaji wa Ujerumani, Andre Schurrle hakuwepo kwenye kikosi cha Chelsea na kufanya tetesi za kuhama kwake zipewe uzito sasa. Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Cech, Christensen, Zouma, Cahill, Azpilicueta, Ramires, Mikel/Fabregas dk70, Remy/Hazard dk76, Oscar, Salah/Willian dk69 na Drogba.
  Bradford City; Williams, Darby, McArdle, Davies, Meredith, Liddle, Morais/Clarke dk89, Halliday/Routis dk86, Knott/Yeates dk79, Hanson na Stead.
  Yeates (centre on his knees) celebrates scoring the winning goal as his Bradford team-mates enjoy the moment
  Wachezaji wa Bradford wakishangilia ushindi wao leo
  Jose Mourinho (right) exchanges some angry words with his opposite number Parkinson during the first half
  Jose Mourinho (kulia) akijibazana kwa hasira na kocha mwenzake, Parkinson katika mchezo huo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2924602/Chelsea-2-4-Bradford-League-One-fight-two-goals-ruin-Jose-Mourinho-s-chances-historic-quadruple.html#ixzz3PlK3yZdg 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA, MOURINHO WAUMBULIWA NA ‘KITIMU CHA MCHANGANI’, WAPIGWA 4-2 DARAJANI KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top