• HABARI MPYA

  Thursday, May 09, 2024

  MTIBWA SUGAR YAZINDUKA, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Jimson Mwanuke dakika ya 15, Charles Ilamfya dakika ya 55 na Nickson Mosha dakika ya 79.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 20, ingawa inaendelea kushika mkia, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 23 nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAZINDUKA, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top