• HABARI MPYA

  Saturday, May 04, 2024

  ARSENAL YAICHAPA AFC BOURNEMOUTH 3-0 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na washambuliaji Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka kwa penalti dakika ya 45 hilo likiwa bao lake la 16 msimu huu, Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya 70 na kiungo Muingereza, Declan Rice dakika ya  90'+7.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 83 katika mchezo wa 36 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ikifuatiwa na mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 79 na muda huu wapo uwanjani katika mchezo wa 35 wakimenyana na Wolverhampton Wanderers.
  Kwa upande wao AFC Bournemouth baada ya kipigo cha leo wanabaki na pointi zao 48 za mechi 36 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA AFC BOURNEMOUTH 3-0 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top