• HABARI MPYA

  Wednesday, May 01, 2024

  YANGA YAIKANYAGA TABORA UNITED 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 35 na washambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 66 na Muivory Coast, Joseph Guede dakika ya 82.
  Kwa matokeo hayo Yanga inakuwa timu ya tatu kutinga Nusu Fainali ya michuano hiyo baada ya Coastal Unión na Ihefu SC.
  Coastal Union imetinga Nusu Fainali ya CRDB Bank Federation Cup baada ya kuichapa Geita Gold 1-0 leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Nayo Ihefu SC imeitoa Mashujaa FC kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 0-0 leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Katika Nusu Fainali,Yanga itakutana na Ihefu SC, wakati Coastal Unión atakutana na mshindi kati Namungo FC zitakazomenyana Ijumaa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAIKANYAGA TABORA UNITED 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top