• HABARI MPYA

  Sunday, May 05, 2024

  HAALAND APIGA NNE MAN CITY YAICHAPA WOLVES 5-1


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Ilikuwa siku nzuri kwa washambuliaji Mnorway, Erling Haaland aliyefunga mabao manne dakika za 12 kwa penalti, 35,  45'+3 kwa penalti na 54, wakati lingine limefungwa na Muargentina, Julián Álvarez dakika ya 85 na bao pekee la Wolverhampton Wanderers limefungwa na mshambuliaji Mkorea Hwang Hee-Chan dakika ya 53.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 82 katika mchezo wa 35, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Arsenal ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
  Kwa upande wao Wolverhampton Wanderers baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 46 za mechi 36 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA NNE MAN CITY YAICHAPA WOLVES 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top