• HABARI MPYA

  Tuesday, May 07, 2024

  CRYSTAL PALACE YAITWANGA MAN UNITED 4-0 SELHURST PARK


  WENYEJI, Crystal Palace wameipa kipigo kizito Manchester United cha mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.
  Kiungo wa umri wa miaka 22, Michael Akpovie Olise amefunga mabao mawili dakika ya 12 na 66, huku mabao mengine yakifungwa na Mfaransa mwenzake, mshambuliaji Jean-Philippe Mateta (26) dakika ya 58 na beki Muingereza, Tyrick Kwon Mitchell (24) dakika ya 66.
  Kwa ushindi huo, Crystal Palace wanafikisha pointi 43 katika mchezo wa 36 nafasi ya 14, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao 54 za mechi 35 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CRYSTAL PALACE YAITWANGA MAN UNITED 4-0 SELHURST PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top