• HABARI MPYA

  Saturday, May 25, 2024

  YANGA SC YAENDELEZA UMBWAMBA LIGI KUU, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0

  MABINGWA mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Gnadou Guede dakika ya 19 na viungo, Mkongo Maxi Mpia Nzengeli dakka ya 49 na Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 90’+1.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 77 kileleni ikifuatiwa na Azam FC na Simba SC zenye pointi 66 kila moja, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 27 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu zote kucheza mechi 29. 
  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
  Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAENDELEZA UMBWAMBA LIGI KUU, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top