• HABARI MPYA

  Wednesday, May 08, 2024

  BORUSSIA DORTMUND YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA, PSG NA MBAPPE OUT


  TIMU ya Borussia Dortmund imefanikiwa kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Paris Saint-Germain ya akina Kylian Mbappé usiku huu Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris nchini Ufaransa.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki mkongwe wa umri wa miaka 35, Mats Julian Hummels dakika ya 50 akimalizia kazi nzuri ya Mjerumani mwenzake, kiungo Julian Brandt.
  Kwa matokeo hayo Borussia Dortmund wanakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-0 kufuatia kushinda 1-0 pia kwenye mechi ya kwanza nyumbani Mei 1 bao pekee la kiungo Mjerumani, Niclas Fullkrug Uwanja wa Signal Iduna Park Jijini Dortmund.
  Sasa Borussia Dortmund watakutana na mshindi wa jumla kati ya Bayern Munich ya Ujerumani pia na Real Madrid ya Hispania ambazo zitarudiana kesho Jijini Madrid baada ya sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza Jijini Munich wiki iliyopita.
  Fainali ya UEFA Champions League msimu huu itapigwa Uwanja wa Wembley Jijini London Jumamosi ya Juni 1 mwaka huu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BORUSSIA DORTMUND YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA, PSG NA MBAPPE OUT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top